Kiswahili English

Huduma kuu ya Fasta Cycle Messengers ni kuchukua na kupeleka barua, vifurushi na mizigo kutoka kwa ofisi au sehumu moja mpaka sehemu nyingine ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Kwa hiyo, huduma zetu ni:

  • mara moja, siku ile ile - mteja anahitaji kifurushi kichukuliwa leo na kipelekwe leo leo
  • mara moja, taarifa kabla - mteja anaagiza kifurushi kichukuliwe na kipelekwe kesho au baadaye
  • mara kwa mara, mfano kupeleka magazeti au vifurushi vingine kila siku au kila wiki
  • kusafirisha bidhaa kubwa - kwa maguta baadala ya baisikeli ya kawaida
  • kuchukua barua kutoka kwa sanduka la posta la mteja mpaka ofisi ya mteja
  • huduma za mkataba kutoka kwa kampuni za courier za kitaifa au za kimataifa

Huduma zingine ni:

  • huduma za kufuatilia, mfano kukaa foleni kwa ajili ya mteja, kufuatilia jibu la barua ofisini kwa ajili ya mteja.
  • huduma za promotion mfano kusambaza vipeperushi
  • kutangaza kwa kuweka matangazo kwenye gurudumu ya nyuma ya baisikeli zetu

Fasta tunafuata taaribu za kufuata kifurushi chako kutoka kwa sehemu ya kuchukua hadi sehemu ya kupeleka, na kupata saini ya anayepokea.