Kiswahili English

Kwetu Fasta, "maeneo ya kati kati" ina maana ya kati kati ya mjini, Kariakoo na Upanga. Ila huduma iwe ndani ya maeneo haya, lazima sehemu ya kuchukua na pia sehemu ya kupeleka pawe ndani ya maeneo ya kati kati. Huduma ya siku ile ile maana mteja anatupa taarifa leo na anahitaji huduma leo. Huduma ya taarifa mapema maana yake mteja ametupa taarifa leo na anahitaji huduma kesho au baada ya kesho.

Huduma ya siku ile ileHuduma ya taarifa mapema
Ndani ya maeneo ya kati katiTsh 3,000Tsh 2,000
Nje ya maeneo ya kati kati, chini ya 10kmTsh 6,000Tsh 5,000
Nje ya maeneo ya kati kati, zaidi ya 10km kati ya sehemu ya kupokea kifurushi mpaka sehemu ya kupeleka kifurushiTsh 10,000Tsh 9,000

Kama mizigo ina thamani ya zaidi ya Tsh 50,000, kuna ada ya ziada ya 2% ya thamani ya mizigo.

Kama kuna kazi ya ufuatiliaji ambayo inaweza kuchukua zaidi ya nusu saa, mfano kukaa foleni ofisini, kusubiri jibu n.k., kuna ada ya ziada ya Tsh 3,000

Kama kuna kazi ya kurudisha karatasi ya jibu/risiti n.k. kutoka anayepokea kifurushi mpaka anayetuma kifurushi, kuna ada ya ziada ya Tsh 3,000.

Kwa huduma za kila mara kwa mara, huduma za mizigo kubwa inayosafirishwa na maguta baadala ya baisikeli, huduma za kupeleka vifurushi sehemu mbali mbali na huduma zingine tafadhali wasiliane nasi kujua bei.