Kiswahili English

Fasta Cycle Messengers tunatoa huduma za kutegemea na tunafuata taaratibu kuhakikisha kifurushi chako kiwe salama. Kama kifurushi chako kinapotezwa au kinaharibika/kinavunjikwa, tutalipa fidia ya thamani ya kifurushi chako, kama umetupa taarifa ya thamani yake kabla ya huduma. Kama kifurushi kina thamani ya zaidi ya Tsh 50,000, kuna ada ya ziada kama inavyoeleza kwenye kurusa ya "bei zetu" kwenye tovuti hii. Fasta italipa fidia ya thamani ya kifurushi chenyewe tu na haitalipa fidia ya usumbufu, kupoteza biashara n.k..