Kiswahili English

Fasta Cycle Messengers tunatoa huduma ya kuchukua na kuleta barua, vifurushi na mizigo kutoka sehemu moja mpaka sehemu nyingine ndani ya Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa chombo kinachotumia nguvu ya mtu (kisichotumia moto wala mafuta) hasa baisikeli na guta. Fasta ni ushirika, maana ni wapanda baisikeli wenyewe ambao ni wenye hisa na ambao wanaendesha shughuli za ushirika. Fasta ilianzishwa na Umma wa Wapanda Baisikeli Dar es Salaam (UWABA), NGO ya wapanda baisikeli wa Dar es Salaam, na uanzishaji uliwezeshwa na shirika lijulikanalo kama International Centre for Sustainable Cities.

Fasta Cycle Messengers tunatoa huduma za haraka na kwa kutegemeka za "courier" ndani ya mkoa ya Dar es Salaam. Wapanda baisikeli wetu wanaweza kupeleka barua, vifurushi na mizigo yako kutoka mlango hadi mlango, na kutoa huduma zingine. Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu huduma zetu kwenye tovuti hii.

Fasta Cycle Messengers inatambulika kiserikali tuko chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Fasta Cycle Messengers ni ushirika ambao umesajiliwa chini ya sheria ya Cooperative Societies Act No 20 ya mwaka 2003.

Wakati wa kutumia huduma za Fasta Cycle Messengers, pia unapata faida ya kusaidia mradi wa mapato kwa wapanda baisikeli wanaoishi kwenye hali ngumu, pia unasaidia mazingira kwa kupunguza uchafuzi wa hewa na utoaji wa carbon kwa kutumia usafiri wa sio ya moto jijini Dar es Salaam.